Sunday, December 15, 2024

COMPETENCY-BASED CURRICULUM IN KENYA: GRADES 7 TO 9



COMPETENCY-BASED CURRICULUM IN KENYA: GRADES 7 TO 9

 

Kenya's education system was altered with the introduction of the Competency-Based Curriculum. Replacing the traditional 8-4-4 system, CBC focuses on skills, attitude, and application of knowledge rather than rote memorization. It aims at preparing the learner to face challenges of the 21st century by fostering the development of individual talents, critical thinking, and problem-solving. The Junior Secondary School phase, comprising Grades 7 to 9, is a vital component of this system, acting as a transition point where learners deepen their understanding, explore diverse disciplines, and build on foundational skills acquired in earlier grades.

CURRICULUM STRUCTURE AND OBJECTIVES

 

In the CBC framework, Grades 7 to 9 focus on molding learners' talents and preparing them for advanced education and careers. The curriculum provides opportunities to explore multiple learning areas while promoting holistic development. Core subjects include Mathematics, English, Kiswahili, Science, Social Studies, and Religious Education. Additionally, optional subjects such as visual arts, music, home science, and technical education allow learners to pursue interests and talents.

 

Key objectives at this stage are the development of critical thinking, collaboration, and fostering creativity. Learners are normally involved in practical activities, group projects, and research-based tasks that emphasize the use of knowledge in real situations. 

 

The Role of Pathways in CBC

A unique element of Grades 7 to 9 is the pathways that take learners into specializations and fields of interest and aptitude. The three pathways are:

1. Arts and Sports Science

   This is for learners who have talent and interest in creative and sporting disciplines. It has subjects such as visual arts, performing arts, music, and physical education.

2. Social Sciences

   With a focus on humanities, this strand encompasses such disciplines as geography, history, religious studies, and social ethics.

3. Science, Technology, Engineering, and Mathematics (STEM)

 

   For learners leaning toward technical and scientific fields, this strand encompasses advanced mathematics, applied sciences, and computer studies.

 

Pedagogical Approaches

The CBC focuses on the following learner-centered teaching approaches:

 

- Project-Based Learning: Learners work on projects that require research, teamwork, and problem-solving, often culminating in presentations or prototypes. 

- Inquiry-Based Learning: This approach encourages learners to ask questions, investigate solutions, and build knowledge through exploration. 

- Practical Assessments: Emphasis is placed on hands-on activities, such as experiments, artistic creations, and technical tasks, to enhance learning by doing.

These strategies ensure that the learners acquire both theoretical understanding and practical skills and attitudes necessary for personal and societal development.

Assessment in CBC

The CBC adopts a continuous assessment instead of an over-reliance on standardized examinations. Learners are thus assessed based on their performance in class activities, projects, portfolios, and formative assessments. By the end of Grade 9, learners undergo summative assessment to determine if they are ready for engagement in Senior Secondary School. Besides, the assessment is accompanied by a record of performance of the learner in different subjects and co-curricular activities.

The shift in assessment methods means that there is less pressure resulting from examinations and that assessments will give a more actual reflection of the capability of a learner and his progress. 

 

Challenges in Implementing CBC for Grades 7 to 9 

 

While CBC has its merits, it faces numerous challenges that are prevalent in Kenya. These are: 

 

1. Infrastructure: Some schools do not have prior facilities such as laboratories, workshops, and libraries to execute practical learning.

 

2. Training of Teachers: Not all teachers undergo complete training on CBC approaches, and at times this negatively reflects in teaching.

3. Parental Engagement: The curriculum demands parental involvement in supporting learning even at home, which could be an uphill task for some families, either because of the pressures of modern life or other resources constraints.

4. Resource Availability: Learning materials, including textbooks and equipment for practical lessons, are often inadequate or maldistributed.

5. Equity Issues: Rural and less-well-off schools face challenges in meeting the demands of CBC owing to a lack of funding and infrastructure gaps.

The Way Forward

In light of these challenges, the Kenyan government and stakeholders have taken the following measures, among others:

- More money invested in the infrastructural development of schools.

- More frequent training for teachers on how to deliver CBC.

- Sensitization for parents on their role in the new education system.

- Collaboration with private companies in resource and technological provision for disadvantaged schools.

Conclusion

The CBC for Grades 7 to 9 represents a bold step in the direction of a more inclusive, practical, and skills-based education system in Kenya.

In focusing on the holistic development of learners, it aims at creating future-ready individuals who can thrive in varied fields. However, this sustained effort calls for investment and collaboration by all stakeholders to overcome the challenges in the implementation of the CBC. As Kenya continues on this transformative journey, the Junior Secondary phase remains a cornerstone in shaping the nation’s educational landscape.


Thursday, August 4, 2022

TUSHANGILIE KENYA

 

TUSHANGILIE KENYA

 tushangilie kenya taifa letu tukufu

 kenya tunayoipenda daima

 kenya nchi tunayoipenda daima

 twajivunia sana tukijiita wa kenya

 nchi yenye baraka Daima

  kenya nchi yenye baraka daima 

 tumekomboa kenya taifa letu tukufu

 tumebadili mwendo daima

Tunalinda katiba mpya daima

 anayependa kenya ni yule mwenye kutenda haki kwa watu wote daima 

mtu mwenye kutenda haki Daima

 na ukipenda kenya ujitengane na mambo yenye kuvunja amani Daima

 hatutaki matata kenya daima 

Wenye nchi

 kenya kipenzi chetu

 Hatutaiacha milele Daima

Wenye nchi 

Kenya kipenzi chetu hatutaiacha milele daima 

Kenya kipenzi chetu nchi yenye upendo

 hatutaacha kenya daima na milele

 kenya kipenzi chetu hatutaiacha milele daima

 wenye  nchi

 kenya kipenzi chetu hatutaiacha milele daima

 nani kiendaa nje

 sitasahau kenya  na nitabaki mkenya daima na milele

kenya kipenzi chetu

 hatutaiacha milele daima

 Mwenye nchi

 kenya kipenzi chetu hatutaiacha milele daima 

na tumeapa sote Wenye nchi  ya kenya

 kutumikia kenya daima na milele

 kenya kipenzi chetu

 hatutaiacha milele daima

 wenye nchi

 kenya kipenzi chetu

 hatutaiacha milele daima

Sitaiacha kenya nchi yangu

 mimi ni mwenye kenya daima

 umoja wetu kenya tudumishe

 mimi mwenyewe kenya daima

 sitadanganywa  kamwe na porojo

 mimi ni mwenye kenya daima

 yenye kuleta chuki kati yetu

 mimi mwenye kenya daima

 nitatetea haki za wakenya

 mimi ni mwenye kenya daima

wala sitakubali ukabila

 mimi ni mwenye kenya daima

  sitaharibu mali ya wengine

Mimi mwenye kenya daima

 na majirani wangu nitalinda 

 mimi mwenye kenya daima

 wenye nchi wenzanguu

 kenya kipenzi chetu

 hatutaiacha milele daima

 wenye   nchi

 kenya kipenzi chetu

 hatutaiacha milele daima

 tushangilie kenya taifa letu tukufu

 kenya tunayoipenda daima

 kenya tunayoipenda daima

 kenya nchi tunayoipenda daima  





Friday, August 27, 2021

458 VITENDAWILI VYA KISWAHILI NA MAJIBU YAKE/ RIDDLES IN ENGLISH

 VITENDAWILI VYA KISWAHILI NA MAJIBU YAKE/ RIDDLES IN ENGLISH



  1. 1.  
  2. Anatega huku akitamba- boga
  3. 2.   Afuma na hana mshale- nungu,nungunungu.
  4. 3.   Adui popote uendapo yuko nawe- nzi,inzi
  5. 4.   Ajenga ingawa hana mikono – nyuni/ndege
  6. 5.   Anajifunua huku akijifunga – mwamvuli/ mwavuli
  7. 6.   Akitokea watu wote humwona- jua
  8. 7.   Akitoka mkewe na wanawe hulala -jua
  9. 8.   Akitokea watu wote humwona na kuwa nan a huzuni- ndwele/ugonjwa.
  10. 9.   Akivaa nguo hapendezi, akiwa uchi yuapendeza mno- ndizi/mgomba
  11. 10.                    Alipita mtu mwenye kibandiko cha nguo- inzi/nzi
  12. 11.                    Alipita mtu ana bunda la mshale – mkindu
  13. 12.                    Aliliwa, yuala, ala, aliwa- papa
  14. 13.                    Amchukuapo hamrudishi- kaburi
  15. 14.                    Amefunika kote kwa blanketi lake jeusi- giza
  16. 15.                    Aamkapo mtu husema hivi: yuaa! Kupiga miayo
  17. 16.                    Abeba mishale aendapo- nungunungu au kalunguyeye
  18. 17.                    Abiria wate wamelipa ila hawa weusi – nzi
  19. 18.                    Adona wala hamezi – mashini ya kupigia chapa
  20. 19.                    Adui hatari; sote tumemzingira lakini hatuwezi kumshika- moto na wanaouota
  21. 20.                    Adui mpenzi-  moto
  22. 21.                    Adui wa wengi lakini humwepuki popote uendapo- nzi
  23. 22.                    Adui wangu haniwahi- handaki(m.y.k: mfereji au shimo kubwa)
  24. 23.                    Aenda m bio ingawa hana miguu –nyoka
  25. 24.                    Afahamu kuchora kalini hajui akichoracho – konokono
  26. 25.                    Akamatwapo mkiani huitii amri- kata(kifaa cha kuchotea maji)
  27. 26.                    Akifa anajizomea-kifuu(ganda la nazi)
  28. 27.                    Akikaa hafi wala akilala hafi-jiwe
  29. 28.                    Akikosekana maana inakosekana-kamsi
  30. 29.                    Akikuandama hupendwi-ukoma
  31. 30.                    Akila yeye na mimi hushiba-mtoto tumboni
  32. 31.                    Akinyamaza hawezi tuongea tena- maiti
  33. 32.                    Akiona mwangaza wa jua yuafa- samaki
  34. 33.                    Akiondoka hawezi kurudi- jani la mti
  35. 34.                    Akiongea kila mtu hubabaika-radi
  36. 35.                    Asubuhi hucheka mchana hukasirika -umande
  37. 36.                    Akishazaa yeye hufariki –kinyonga
  38. 37.                    Akitambaa huringa hata akiwa hatarini – jongoo
  39. 38.                    Akitoa sauti yake, wote hutafuta pa kujificha – mauti
  40. 39.                    Akitoka mkewe na watoto hulala-jua
  41. 40.                    Akitokea watu wate humwona-jua
  42. 41.                    Akitokea watu watu wote hunung’unika na kuwa na huzuni- ugonjwa
  43. 42.                    Akopa na halipi.  Kaburi
  44. 43.                    Alia pasipo kupigwa – mgonjwa wa macho
  45. 44.                    Alianika mpunga wake alipoamka haupo-nyota
  46. 45.                    Alimsimamisha jumbe njiani – chawa
  47. 46.                    Alikwenda kwa mjomba hakurudi- jani liloanguka
  48. 47.                    Alinipa ngozi nikaipika, akanipa nyama nikaila akanipa mchuzi nikaunywa- nazi
  49. 48.                    Ialipita mtu mwenye kibandiko cha nguo nazi
  50. 49.                    Alipita mtu na bunda la mishale- mkindu
  51. 50.                    Aliyechuma hakula, aliyekula hakumeza,aliyemeza hakushiba- mkono, kinywa na koo
  52. 51.                    Aliyefuatwa amekuja; bali aliyefuata hajaja –nazi na mkwezi
  53. 52.                    Aliyenunua hakutumia, aliyetumiahakuiona-sanda(kitamba cha kufunika maiti)
  54. 53.                    Amchukuapo hamrudishi –kaburi
  55. 54.                    Amechana hakushona- jani la mgomba hupepea na kuchanika
  56. 55.                    Amafungua  macha lakini haoni- sungura awapo usingizini
  57. 56.                    Amefunua jicho jekundu –jua
  58. 57.                    Amenukia kote kwa blanketi lakini jeusi- giza
  59. 58.                    Amejaa ulafi tele hivi kwamba daima hashibi =mchanga
  60. 59.                    Amekaa kimya na watoto wamemzunguka pande zote –mgomba
  61. 60.                    Amakula ncha mbili – wali
  62. 61.                    Ametanda kote kwa vazi lake jeusi- giza totoro
  63. 62.                    Amevaa joho kubwa kuliko yeye mwenyewe –kaburi
  64. 63.                    Amezaliwa ali, amekufa ali na amerudi ali –nywele
  65. 64.                    Ana blanketi nyingi lakini hawafuniki wanawe – mboga
  66. 65.                    Ana macho lakini haoni –popo
  67. 66.                    Ana mali nguo havai –kinu
  68. 67.                    Ana meno lakini hayaumi kitana/chanuo(kichanuo)
  69. 68.                    Ana mikono lakini hawezi kushika kitu- ndege
  70. 69.                    Ana nguvu na uwezo kutushinda sote- mungu
  71. 70.                    Anakuangalia tu wala halali au kutembea  -picha
  72. 71.                    Anakula  chakula cha afya hali hanoni –sufuria
  73. 72.                    Anakula kila siku lakini hashibi wal hatashiba –mauti
  74. 73.                    Anakula lakini hashibi- mauti
  75. 74.                    Anakwenda anadeka anaruka –ng’ombe
  76. 75.                    Anamea tu bali hana faida nywele
  77. 76.                    Ananyweshwa kila wakati, lakini hatosheki –bahari
  78. 77.                    Anaoga kila wakati lakini hatakati –chura
  79. 78.                    Anaota moto kwa mgongo – chungu
  80. 79.                    Anapendeza akinguruma - chungu
  81. 80.                    Anapenda kujitwisha mzigo mzito kuliko alivyo mwenyewe –kaa/konokono
  82. 81.                    Anapenda sana kutrmbea na kila arejeapo nyumbani humwamba mama amweleke- mtu na kitanda
  83. 82.                    Anapendwa sana ingawaje mkali sana –mto
  84. 83.                    Anapokuchukuwa hakurudishi –kaburi
  85. 84.                    Anasema kula hali –redio
  86. 85.                    Anataga huku akitembea –mboga
  87. 86.                    Anatembea nawe lakini ni adui mkubwa bakora
  88. 87.                    Ashinda akicheka –fisi
  89. 88.                    Amekata mti akauwacha ukitoa moshi –mavi
  90. 89.                    Anazurura mwituni na pikipiki nyekundu –damu mwilini
  91. 90.                    Alimsimamisha jumbe njiani – chawa
  92. 91.                    Aspro juu ya mti –mavi ya ndege
  93. 92.                    Akivaa miwani hafanyi kazi vizuri- mlevi
  94. 93.                    Akinishika tu ninazaa- mfereji
  95. 94.                    Apendeza tu akiwa uchi- mahindi
  96. 95.                    Anitengenezaye hana haja name, aninunuaye hanitumii. Naye anitumiaye hanioni kamwe. Je mimi ni nani? Jeneza
  97. 96.                    Askari wangu watoapo kofia wafanyi kazi tena- njiti(match stick)
  98. 97.                    Iaskari wangu wamevaa vilemba vyekundu na wengine vyeusi –niti za kiberiti
  99. 98.                    Askari wa ng’ombe mtembezi –kivumanzi(kengele ya kufungia kwa wanyama)
  100. 99.                    Askari tele mzungu katikati – meno na ulimi
  101. 100.              Askari wanalinda njia huku na huku-milango ambayo ipo barazani/uani
  102. B
  103. 101.              Ba funua ba funika – unyayo
  104. 102.              bak bandika bak bandua -nyayo
  105. 103.              Baba alinika mfupa nikautunza ukawa fahali -muwa
  106.                             


VITENDAWILI  SEHEMU YA PILI

  1.Adui lakini po pote uendako yuko nawe. Inzi
2.                  Afahamu kuchora lakini hajui achoracho. Konokono
3.                  Afuma hana mshale. Nungunungu
4.                  Ajenga ingawa hana mikono. Ndege
5.                  Ajifungua na kujifunika. Mwavuli
6.                  Akitokea watu wote humwona. Jua
7.                  Akitokea watu wote hunungunika na kuwa na huzuni. Ugonjwa
8.                  Akivaa nguo hapendezi, akiwa uchi apendeza. Mgomba
9.                  Alipita mtu ana bunda la mshale. Mkindu
10.              Alipita mtu mwenye kibandiko cha nguo. Inzi
11.              Aliwa, yuala; ala, aliwa. Papa
12.              Amchukuapo hamrudishi. Kaburi
13.              Amefunika kote kwa blanketi lake jeusi. Giza
14.              Amefunua jicho jekundu. Jua
15.              Ameingia shimoni akiwa uchi, akatoka amevaa nguo nzuri. Mbegu
16.              Amejitwika mzigo mkubwa kuliko yeye mwenyewe. Konokono/Koa
17.              Amekaa kimya na watoto wamemzunguka pande zote. Mgomba
18.              Amekula ncha mbili. Wali
19.              Amevaa joho kubwa kuliko yeye mwenyewe. Kaburi
20.              Anakuangalia tu wala halali au kutembea. Picha
21.              Anakula kila siku lakini hashibi na hatashiba. Mchanga
22.              Anakula lakini hajashiba na hatashiba milele. Ardhi
23.              Anakula lakini hashibi. Mauti
24.              Anapendwa sana ingawaje ni mkali sana. Moto
25.              Anatoka kutembea, anakuja nyumbani anamwambia mama, ‘Nieleke’. Kitanda
26.              Ashona mikeka wala hailali. Maboga
27.              Askari wangu wote wamevaa kofia upande. Majani
28.              Askari wangu wote wamevaa mavazi meusi. Chunguchungu
29.              Asubuhi atembea kwa miguu mine, adhuhuri kwa miwili. Fedha
30.              Atapanya mbegu nyingi sana lakini hazioti. Mvua
31.              Atolewapo nje hufa. Samaki
B
32.           Baba alinipa mfupa, nikautunza ukawa fahali. Muwa
33.           Baba ameweka mkuki nje nikashindwa kuukwea, mdogo wangu akaukwea. Sisimizi
34.           Babako akojoapo hunung’unika. Mawingu
35.           Babu amefunga ushanga shingoni. Mtama/Nazi
36.           Babu anakula ng’ombe, analea fupa linakuwa ng’ombe. Muwa
37.           Babu hupiga kelele akojoapo. Mvua
38.           Babu mkubwa ameangushwa na babu mdogo. Mti na shoka
39.           Babu, nyanya, mjomba, mama, baba na watoto, mna safari ya wapi? Siafu
40.           Bak bandika, bak bandua. Nyayo
41.           Bawabu mmoja tu asiyeogopa chochote duniani. Mlango
42.           Bibi kikongwe apepesa ufuta. Kope za macho
43.           Bibi yake hutandikwa kila siku, lakini hatoroMoyoKinu cha kutwangia

C
44.           Chakula kikuu cha mtoto. Usingizi
45.           Cha ndani hakitoki nje, cha nje hakiingii ndani. Nyama na mfupa
46.           Chang’aa chapendeza, lakini hakifikiwi. Jua
47.           Chatembea na hakijapata kupumzika hata nukta moja. Mwezi/Jua
48.           Cheupe chavunjika manjano yatokea. Yai
49.           Chumba change kina ukuta niondoa na kuusimika nitakapo. Pazia
50.           Chungu change cha udongo hakipasuki kikianguka. Mjusi/Panya
51.           Chungu kikubwa sana chenye kifuniko kikubwa sana. Dunia na mbingu

D
52.           Dada yangu akitoka kwao harudi kamwe. Jani likwanyukapo
53.           Dada yangu kaoga nusu. Jiwe mtoni
54.           Drrrrrh1 Ng’ambo. Daraja la buibui
55.           Dume wangu amelilia machungani. Radi

F
56.           Fahali wa ng’ombe na mbuzi wadogo machungani. Mwezi na nyota angani
57.           Fika umwone umpendaye. Kioo
58.           Fuko kajifukia, mkia kaacha nje. Kata mtungini
59.           Funga mizigo twende Kongo. Mikia ya mbwa

H
60.           Hachelewi wala hakosei safari zake. Jua
61.           Haina miguu wala mikono, lakini, yabeba magogo. Maji
62.           Hakihitaji maji, wala udongo, wala chakula; lakini chamea. Nywele
63.           Hakionekani wala hakishikiki. Hewa
64.           Hakisimami, na kikisimama msiba. Moyo
65.           Hakuchi wala hakuchwi. Kula
66.           Halemewi wala hachoki kubeba. Ardhi
67.           Hamwogopi mtu yeyote. Njaa
68.           Hana mizizi, nimemkata mara nyingi lakini haachi kukua. Ukucha
69.           Haoni kinyaa. Mvua
70.           Hapo nje panapita mtu mwenye miguu mirefu. Mvua
71.           Hasemi, na akisema hatasahaulika. Kalamu
72.           Hasimamishwi akiwa na ghadhabu. Upepo
73.           Hata inyeshe namna gani haifiki humu. Kwapani
74.           Hata jua likiwaka namna gani hakauki wala kupata joto. Pua ya mbwa
75.           Hata Mzungu ameshindwa. Mauti
76.           Hauchagui chifu wala jumbe. Utelezi
77.           Hausimiki hausimami. Mkufu
78.           Hawa wanaingia hawa wanatoka. Nyuki mzingani
79.           Hesabu haihesabiki. Nyota
80.           Huitumia kila siku lakini haiishi. Miguu
81.           Huku kutamu, huku kutamu, katikati uchungu. Jua
82.           Huku unasikia ‘pa’ Huku unasikia ‘pa! Mkia wa kondoo
83.           Hula lakini hashibi. Sindano
84.           Hulala tulalapo, huamka tuamkapo. Jua
85.           Humu mwetu tuko wanne tu, ukimwona wa tano mwue. Matendegu ya kitanda
86.           Huna macho lakini wakamata wanyama. Ndoana
87.           Hupanda mtini na mwenye kichaa wake. Kivuli
88.           Hutembea watatu. Mafiga
89.           Hutoka upesi sana lakini hasalimu. Kuku
90.           Huwafanya watu wote walie. Moshi
91.           Huwezi kukalia alipokalia msichana wangu mweusi. Chungu jikoni
92.           Huzikwa mmoja, hufufuka mmoja, huzeeka wengi. Mbegu na matunda

I
93.           Inaonekana mara mbili katika dakika moja na mara moja tu katika mwaka. Herufi "K"
94.           Ini la ng’ombe huliwa hata na walioko mbali. Kifo

J
95.           Jembe la Wangoni haliishi. Miguu/Nyayo
96.           Je, unaweza, kukua ukampita mzee wako? Nywele kichwani
97.           Jiwe litoalo maji. Macho

K
98.           Kaburi la mfalme lina milango miwili. Kata ya kuchukulia Maji kichwani
99.           Kaka yangu anapanda darini na fimbo nyuma. Paka na mkia wake
100.       Kama kingekuwa mkuki, ungekuta kimekwisha kuua wote. Kizingiti cha mlango
101.       Kama unapenda, mbona usile? Ulimi
102.       Kanipa ngozi nikapikia, kanipa nyama nikala, kanipa mchuzi nikanywa, kanipa mfupa   nikautumia. Nazi
103.       Kapanda mti pamoja na uchawi wake. Tumbaku inaponuswa puani
104.       Kidimbwi kimezungukwa na majani. Macho
105.       Kikioza hutumiwa, kikiwa kichungu hakitumiwa. Maziwa
106.       Kila linapofika kwetu hutanguliza makelele. Mvua
107.       Kila mtu atapitia malango huo. Kifo
108.       Kila mtu hata mfalme huheshimu akipita. Mlango
109.       Kila siku hupita njia hiyo hiyo bali arudipo hatumwoni. Jua
110.       Kileee! Hiki hapa. Kivuli
111.       Kilimsimamisha chifu njiani. Chawa
112.       Kina mikono na uso lakini hakina uhai. Saa
113.       Kinaniita lakini sikioni. Mwangwi
114.       Kisima cha Bimpai kina nyoka muwai, ndiye fisadi wa maji. Taa ya utambi
115.       Kisima kidogo kimejaa changarawe. Kinywa na meno
116.       Kitendawili change ukikitambua nitakupa hirizi. Mimba
117.       Kiti cha dhahabu hakikaliwi na watu. Moto
118.       Kiti cha Sulatni hukaliwa na mwenyewe. Kuku aatamiapo mayai
119.       Kiti nyikani. Uyoga
120.       Kitu changu asubuhi chatembea kwa miguu mine, saa sita kwa miguu miwili, jioni kwa miguu mitatu. Maisha ya binadamu
121.       Kiwanja kizuri lakini hakifai kuweka mguu. Kipara
122.       Kombe ya Sultani Ii wazi. Kisima
123.       Kondoo wangu amezaa kwa paja. Mhindi
124.       Kondoo wangu mnene kachafua njia nzima. Konokono
125.       Kondoo za mtoto zamaliza mavuno. Jiwe la kusagia
126.       Kufanya kwa ridhaa mojamoja. Kusuka mkeka
127.       Kuku wangu aliangua mayai jana, lakini si kuku wala ndege. Nyoka au samaki
128.       Kuku wangu amezalia miibani. Nanasi au chungwa
129.       Kuku wetu hutagia mayai mikiani. Matunda
130.       Kuna mlima mmoja usio pandika. Nafasi kati mdomo na pua
131.       Kuna mtu mwenye tumbo kubwa aliyesimama nje. Ghala
132.       Kuna ziwa kubwa ambalo limekauka na limebakiza mizizi. Chongo
133.       Kunguru akilia hulilia mirambo. Mtoto akililia maziwa
134.       Kwenye msitu mkubwa Napata mti mmoja tu, lakini kwenye msitu mdogo naweza kupata miwili. Watoto wa ng'ombe na mbuzi
135.       Kwetu mishale na kwenu mishale. Mikia ya panya
136.       Kwetu twalala tumesimama. Nguzo za nyumba

L
137.       La mgambo limelia wakatoka weusi tu. Chunguchungu
138.       Likienda hulia, likirudi halilii. Debe aka buyu
139.       Likitoka halirudi. Neno
140.       Liwali amekonda lakini hana mgaga. Sindano


M
141.       Mama ametengeneza chakula lakini hakula. Chungu cha kupikia
142.       Mbona kinakumeza lakini hakikuli? Nyumba
143.       Mbona mwakunjiana ngumi bila kupigana? Mafiga
144.       Mbona mwasimama na mikuki, mwapigana na nani? Katani
145.       Mchana ‘ti’ usiku ‘ti’. Mlango
146.       Mdogo lakini humaliza gogo. Mchwa
147.       Mfalme amesimika mkuki wake hapa name nikausimika wangu kando yake, baadaye
           hatukuitambulisha tena. Kohozi
148.       Mfalme hushuka kwa kelele. Mvua
149.       Mfalme katikati lakini watumishi pembeni. Moto na mafiga
150.       Mfalme wetu hupendwa sana, lakini wakati wa kumwona lazima umtoe nguo zote kwanza. Hindi
151.       Mhuni wa ulimwengu. Inzi
152.       Mkanda mrefu wafka mpaka pwani. Njia
153.       Mke wangu mfupi, lakini huvaa nguo nyingi. Hindi
154.       Mlango wa nyumba yangu uko juu. Shimo la mchwa
155.       Mlima mkubwa wapandwa kuanzia juu. Sima/Ugali
156.       Mlimani sipandi. Maji
157.       Mlima umezuia kutazama kwa mjomba. Kisogo
158.       Mlima wa kupanda kwa mikono. Mlima
159.       Mlima wa kwetu hupandwa na mfalme. Nafasi kati ya mdomo na pua ya ngombe
160.       Mlima wa mwenyewe hupandwa na mwenyewe. Buibui na utando wake
161.       Mpini mmoja tu lakini majembe hayahesabiki. Mkungu wa ndizi
162.       Msitu ambao haulii hondohondo. Mimba
163.       Mti mkubwa, lakini una matawi mawili tu. Kichwa na masikio
164.       Mti mnyanya mti kerekeche mti ah mti ah!. Ngoma na upatu
165.       Mti wangu una matawi kumi na mawili na kila tawi lina majani kadiri ya thelathini. Mwaka
166.       Mtoto asemea pangoni. Ulimi mdomoni
167.       Mtu mdogo mwenye miguu mirefu ambaye aweza kutembea dunia nzima kwa dakika tano. Mawazo
168.       Mvua hema na jua hema. Kobe
169.       Mvua kidogo ng’ombe kaoga kichwa. Jiwe
170.       Mwadhani naenda lakini siendi. Jua
171.       Mwalimu analala na mwanafunzi wanamsomea. Kinyesi na inzi
172.       Mwanamke mfupi hupiga kelele njiani. Kunguru
173.       Mwanamke mfupi hutengeneza pombe nzuri. Nyuki
174.       Mwanang’ang’a hulia mwituni. Shoka
175.       Mwepesi, lakini aweza kuvunja nyumba za mji wote. Tufani
176.       Mwezi wangu umepasuka. Kweme
177.       Mzee Kombe akitoa machozi wote hufurahi. Mvua
178.       Mzee Kombe akilia watu hufurahi. Mvua
179.       Mzizi wa miti hutokea mbali. Siafu
180.       Mzungu yuko ndani na ndevu ziko nje. Hindi

N
181.       Naitumia ngazi hiyo kwa kupandia na kushukia. Mwiba
182.       Nakikimbilia lakini sikikuti. Njia
183.       Nakupa lakini mbona huachi kudai. Tumbo
184.       Nakwenda msituni na mdogo wangu, lakini yeye namwacha huko.
185.       Nameza lakini sishibi. Mate
186.       Namkimbiza lakini simkuti. Kivuli
187.       Namlalia lakini halii. Kitanda
188.       Namwomba atangulie lakini hukataa kabisa. Kigino
189.       Nanywa supu na nyama naitupa. Muwa
190.       Napigwa na mvua na nyumba ipo. Matunda ya pua/Kwapa
191.       Natembea juu ya miiba lakini hainichomi. Miiba
192.       Natembea juu ya miiba lakini sichomwi. Ulimi
193.       Natembea na wenzangu lakini tukifika kwenye nyumba mimi hukaa mlangoni. Mbwa
194.       Natengeneza mafuta lakini nimepauka sana. Mzinga was nyuki kwa nje
195.       Natengeneza mbono lakini alama hazionekani. Mzinga wa nyuki
196.       Ndege wengi baharini. Nyota
197.       Ndugu wawili wafanana sana, lakini hawatembeleani. Macho
198.       Ngoja nikumbuke. Boga changa
199.       Ng’ombe wa baba watelemka mtoni. Mawe mtoni
200.       Ng’ombe wa babu huchezea miambani. Mijusi
201.       Ng’ombe za babu zikienda machungani hulia, zikirudi hazilii. Vbuyu
202.       Ng’ombe za babu zinalala na mkia nje.Viazi vitamu udongoni
203.       Ng’ombe wamechanganyika nikakosa wa kwangu. Pesa/Nyayo
204.       Ng’ombe wangu ni weupe kwatoni. Katani
205.       Ng’ombe wangu wote hunywa maji isipokuwa mmoja. Fimbo ya kuchunga
206.       Ngozi ndani nyama juu. Firigisi
207.       Nguo ivaliwayo kila siku isiyoingiwa na chawa. Nyusi
208.       Nikicheka kinacheka, nikinuna kinanuna. Kioo
209.       Nikienda arudi, nikirudi aenda. Kivuli majini
210.       Niiita ‘baba’ huitika ‘baba’. Mwangwi
211.       Nikija kwenye ndege wananifukuza, na nikienda kwenye wanyama hawanitaki. Popo
212.       Nikimpiga huyu huyu alia. Utomvu wa papai
213.       Nikimpiga mambusu. Puliza kidole wakati unapojikwaa
214.       Nikimwita hunijibu nani. Mwangwi
215.       Nikipewa chakula nala bali natema. Shoka
216.       Nikitembea walio wafu huniamkia na walio hai hukaa kimya. Majani makavu na mabichi
217.       Nikitembea yuko, nikikimbia yuko, nikiingia ndani hayupo. Kivuli
218.       Ni kitu gani ambacho kutoa ni kuongeza? Shimo
219.       Nikitupa mshale wangu mchana huenda mbali sana, lakini niutupapo usiku hauendi mbali. Jicho
220.       Nikiwaambia ondokeni hukataa, lakini mjomba akitokea wote hukimbia. Umande na jua
221.       Nilijenga nyumba yangu nikaiacha bila kuiezeka majani; lakini niliporudi nilikuta imekwisha ezekwa majani. Mahindi machanga
222.       Nilijenga nyumba yangu yenye mlango mmoja. Jani la mgomba la nchani
223.       Nilimkata alafu nikamridhia. Kupanda mbegu
224.       Nilimtuma askari vitani akaniletea kondoo mweusi. Fuko
225.       Nilipandia majanini nikashukia majanini. Mwiba
226.       Nilipigwa na tonge la ugali la moto nilipopita msituni. Manyigu
227.       Nilipitisha mkono wangu chini la ardhi, nikamshika beberu mkubwa sana. Kiazi kikuu
228.       Nilipoangalia kwenye magereza ya Wazungu, nikaona wameketi juu ya mabati. Pelele
229.       Nilipofika msituni nilikuta chungu cha pure kinachemka. Mzinga wa nyuki
230.       Nilipoingia Rumi, alitoka mtu na wake kumi; kila mke na tundu kumi, kila tundu na kuku
           kumi; kila kuku na mayai kumi. Mayai, kuku, tundu, wake, kumi kumi kumi. Wangapi
           walikwenda Rumi? Hakuna
231.       Nilipo, juu kuna miiba na chini vivyo hivyo; lakini sichomwi. Ulimi kinywani
232.       Nilipokuwa mchanga nilikuwa na kijikia lakini sasa sinacho. Chura
233.       Nilitembea na mwezangu naye hupita vichakani. Kivuli
234.       Nimechoma fimbo yangu pakabaki pa kushikia tu. Njia
235.       Nimefyeka mitende yote kiungani isipokuwa minazi miwili tu. Masikio
236.       Nimejenga nyumba babu akaihamia kabla mimi sijahamia. Mjusi
237.       Nimekata mti, akaja samba mwekundu akaukalia. Utomvu
238.       Nimekata mti bara ukaangusha matawi pwani. Nzige
239.       Nimekwenda na rafiki yangu kwa jirani, yeye akafika kabla yangu. Sauti ya nziga
240.       Nimemtahiri binti wangu akatoa damu mchana kutwa. Kivuli
241.       Nimempeleka kondoo wangu akatoa damu mchana kutwa. Mgomba
242.       Nimemtuma mtu kumwamkua mtu, yeye amekuja, Yule aliyetumwa hajaja. Kuangua tunda Ana nazi
243.       Nimemwacha mzee kikongwe mtoni anangojea mgeni kulaki. Mtego
244.       Nimempandikiza mti wangu ukapeleka matawi ng’ambo ya mto. Kivuli
245.       Nimesimama mbali nyikani lakini naonekani. Moto
246.       Nimetembea kitambo, kukumbuka sikufunga nyumba. Dirisha Ana ufa
247.       Nimetoka kutembea kutembea, nikashika ng’ombe mkia. Kata
248.       Nimetupa mshale angani wala sitambui utateremsha ndege wa namna gani. Mimba
249.       Nimeweka ndizi yangu, asubuhi siioni. Nyota
250.       Nimezaliwa na mguu mmoja. Uyoga
251.       Nimezungukwa na adui wengi, lakini siumizwi. Ulimi na meno
252.       Nina kijiti change, nizidivyo kukikata ndivyo kizidivyo kuwa kirefu. Maisha
253.       Nina kitu changu kitumiwacho na wengine kuliko mimi. Jina
254.       Nina kitu kizuri sana nyumbani, lakini siwezi kukichukua. Dada
255.       Nina kitu nipendacho ambacho hata baba, mama, dada, kaka hata na mgeni nimpendaye sana siwezi kumwazima. Mke
256.       Nina mwezi ndani ya bakuli. Maziwa
257.       Nina ng’ombe wangu nisipomshika mkia hali majani. Jembe
258.       Nina nyumba yangu imezungukwa na mifupa. Mdomo
259.       Nina pango langu lilojaa mawe. Kinywa
260.       Nina watoto wangu hamsini na wote nimewavisha visibau vyeupe. Kunguru
261.       Nina watoto watatu, mmoja akitoka kazi haifanyiki. Mafiga
262.       Nina badilika umbo langu baada ya kila muda mfupi. Kivuli
263.       Ninachimba mizizi ya mti usio na mizizi. Jiwe
264.       Ninacho, nakitumia, lakini kila nikitumiapo, sikiharibu ila nakipa rangi. Maji na mkojo
265.       Ninakula vitu vyote vinono lakini sikui wala sinenepi. Chungu cha kupikia
266.       Ninakwenda naye na kurudi naye. Kivuli
267.       Ninao mlima ambao una msitu kileleleni tu. Kichwa
268.       Nitokeapo kila mmoja asema namtazama yeye tu. Jua au mwezi
269.       Njia yapitwa siku zote lakini haina alama. Njia ya jua au mwezi
270.       Njoo hapa nije hapo. Kiraka
271.       Nne nne mpaka pwani. Matendegu
272.       Nusu mfu nusu hai. Sungura alalapo
273.       Nyama ndogo imewashibisha wengi wala isiishe. Kinoo
274.       Nyama ya Reale haijai kikombe. Mkufu
275.       Nyanya yako ana huruma kukubeba ulalapo. Kitanda
276.       Nyumba yangu ina makuti tele, lakini mvua ikinyesha huvuja. Mwembe
277.       Nyumba yangu ina milango mingi. Kichuguu
278.       Nyumba yangu ina nguzo moja. Uyoga
279.       Nyumba yangu kubwa, haina mlango. Yai
280.       Nyumba yangu kubwa, haina taa. Kaburi
281.       Nyumba yangu kubwa hutembelewa mgongoni. Konokono

O
282.       Oh! Mwanamke aliyevunja chungu mshangao wake
283.       Ondoka nikae. Maji ya mfereji

P
284.       Paa alipenga hata pua ikapasuka. Mbarika
285.       Palikuwepo watu watatu wakivuka mto. Mmoja alivuka pasipo kukanyaga maji wala kuyaona; wa pili aliyaona maji lakini alivuka bila kuyakanyaga; wa tatu aliyaona na kuyakanyaga alipovuka.
Ni nani hawa? Was kwanza in Mtoto tumboni mwa mamake, was pili ni Mtoto aliyebebwa mgongoni, was tatu ni mama mwenyewe
286.       Panda ngazi polepole. Sima ya ugali
287.       Para hata Maka. Utelezi
288.       Pete ya mfalme ina tundu katikati. Kata ya kuchukulia mizigo
289.       Poopoo mbili zavuka mto. Macho
290.       Po pote niendako anifuata. Kivuli

R
291.       Rafiki yangu ana mguu mmoja. Uyoga
292.       Reli yangu hutandika ardhini. Siafu
293.       Ruka Riba. Maiti

S
294.       Shamba langu kubwa lakini mavuno hayajazi kiganja. Nywele kichwani
295.       Shamba langu miti mitano tu. Mkono wa vidole
296.       Shangazi yangu ni mrefu sana lakini hafikii tumbo la kondoo. Njia
297.       Sijui aendako wala atokako. Upepo
298.       Sijui afanyavyo. Nyoka apandavyo mtini
299.       Sina dada wala kaka, lakini baba wa huyu jamaa ni mtoto wa babangu. Ni nani huyo? Mtoto wangu
300.       Subiri kidogo! Miiba
301.       Sultani alipiga mbiu watu waje kufanya kazi yake lakini wakashindwa. Maji

T
302.       Taa ya bure. Jua au mwezi
303.       Taa ya Mwarabu inapepea. Kilemba
304.       Tajiri aniweka mfukoni na maskini anitupa. Makamasi
305.       Tandika kitanga tule kunazi. Nyota
306.       Tangu kuzaliwa kwake sijamwona asimame wala kukimbia. Mkufu
307.       Tatarata mpaka ng’ambo ya mto. Utando wa baibui
308.       Tatu tatu mpaka pwani. Mafiga
309.       Tega nikutegue. Mwiba
310.       Teke teke huzaa gumugumu, na gumugumu huzaa teke teke. Mahindi ama yai
311.       Tengeneza kiwanja kikubwa kabila Fulani lije kupigania. Mbono
312.       Tonge la ugali lanifikisha pwani. Jicho
313.       Tukate kwa visu ambacho hakitakatika. Maji
314.       Tulikaribishwa mahali na mdogo wangu, yeye akaanza kushiba kabla yangu. Kucha
315.       Tuliua ng’ombe na babu, kila ajaye hukata. Kinoo
316.       Tuliua ng’ombe wawili ngozi ni sawasawa. Mbingu na nchi
317.       Tumvike mwanamke huyu nguo. Kuezeka nyumba
318.       Tunajengajenga matiti juu. Mapapai
319.       Twamsikia lakini hatumwoni. Sauti

U
320.       Ukimcheka atakucheka, ukimwomba atakuomba. Mwangwi
321.       Ukimwita kwa nguvu hasikii, lakini ukimwita polepole husikia. Fisi
322.       Ukimwona anakuona. Jua
323.       Ukitaka kufahamu ana mbio, mwonyeshe moto. Kinyonga
324.       Ukitembea ulimwengu wote utakosa nyayo. Mwamba
325.       Ukiukata haukatiki, ukiushika haushikiki. Moshi
326.       Ukiwa mbali waweza kumwona Fulani umatini. Tundu LA sindano
327.       Ukoo wa liwali hauna haya. Wanyama
328.       Ule usile mamoja. Kifo
329.       Umempiga sungura akatoa unga. Funds LA mbuyu
330.       Unatembea naye wote umjiao atakuona. Bakora
331.       Upande wote umjiao atakuona. Kinyonga
332.       Ushuru wa njia wKujikwaa Kujikwaa
333.       Utahesabu mchana na usiku na hutamaliza kuhesabu. Nywele

V
334.       Viti kumi nyumbani, tisa vyakalika lakini kimoja hakikaliki. Moto

W
335.       Wake wa mjomba kimo kimoja. Vipande vya kweme
336.       Wako karibu lakini hawasalimiani. Nyumba ama kuta zinazoelekeana
337.       Wanakuja mmoja mmoja na kujiunga kuwa kitu kimoja. Matone ya mvua
338.       Wanameza watu jua linapokuchwa. Nyumba
339.       Wanamwua nyoka. Watu wanaotwanga
340.       Wanangu wawili hugombana mchana, usiku hupatana. Mlango
341.       Wanao wakati wao wa kuringa, nao ni weupe kama barafu. Nyota
342.       Wanapanda mlima kwa makoti mazuri meusi na meupe. Vipepeo
343.       Wanastarehe darini. Panya
344.       Wanatembea lakini hawatembelewi. Macho
345.       Watoto wa mtu mmoja hulala chini kila mwaka. Maboga
346.       Watoto wangu wana vilemba, asio kilemba si mwanangu. Fuu
347.       Watoto wangu wote nimewavika kofia nyekundu. Jogoo
348.       Watoto wangu wote wamebeba vifurushi. Vitovu
349.       Watu ishirini walipanda juu ya mti, wawili wakaona chungwa, watano wakalichuma, kumi wakalimenya, wote wakaridhirika mtu mmoja alile. Je, ni watu gani hao? Waliopanda ni vidole vya miguu na mikono, walioona ni macho mawili, waliochuma ni vidole vitano vya mikono, waliomenya ni vidole vya mikono yote miwili, na aliyelila ni mdomo
350.       Watu waliokaa na kuvaa kofia nyekundu. Kuku, katani au mahindi
351.       Watu wamehama askari wekundu wakazidi nyikani. Viroboto
352.       Watu wawili hupendana sana; kati ya mchana hufuatana ingawa mmoja ni dhaifu. Usiku mdhaifu
           haonekani tena. Kivuli
353.       Watu wote ketini tumfinye mchawi. Kula ugali
354.       Wewe kipofu unaenda wapi huko juu? Mkweme

Y
355.       Yaenda mbali lakini haiondoki ilipo. Njia

Z
356.       Zilitazamana na mpaka sasa hazijakutana. Kingo za mto
357.       Ziwa dogo linarusha mchanga. Chungu jikoni

358.       Ziwa kubwa, lakini naogelea ukingoni tu. Moto